Advertisement

MAAJABU YA GOOGLE LENS


 Unajua maajabu ya Google lens kwenye simu zetu? Google lens inaweza kukugeuza mchawi wa teknolojia kwenye simu , utaweza kurahisha mambo mengi kupitia simu yako!!


Inatumia teknolojia ya Artificial intelligence kuweza kutambua ujumbe na vitu Kwa mfumo wa picha pamoja na live view kupitia camera yako, inakusaidia kujifunza jinsi ya kuingiliana navyo kwenye kila njia kuifanya ya kuvutia zaidi.


1️⃣ Copy text from real words

  uwezo wa kuchukua ujumbe kutoka kwenye karatasi, kitabu,shati, ubao, mabango au kitu Chochote kilichoandika au kubandikwa mahali Fulani na kukiweka kwenye simu yako Kwa mfumo wa ujumbe (text) 


Kwaiyo badala ya kuandika kitu Toka mahali Fulani kukiweka kwenye simu we una copy tu 😄.


2️⃣ Send text from real words to your laptop au desktop

Kuna baadhi ya watu hawatumi tu simu pekee pia PC Kuna nyakati Unatumia labda Kuna ujumbe umeupenda mahali unataka kuweka kwenye PC yako basi kupitia Google lens unaweza kuhamisha text kutoka kwenye simu kwenda kwenye PC 


3️⃣ Hear text from the real words

Google lens inakusaidia kwenye kusoma ujumbe mbalimbali chukulia mfano umetumiwa ujumbe mrefu labda unataka kusikiliza badala ya kusoma basi kupitia Google lens inakusaidia kusikiliza maneno yote na pia inakusaidia kuweza kujua baadhi ya maneno yanatamkwaje Kwa usahihi.


4️⃣ interact with text from an image 

Unakua na uwezo wa kuchukua ujumbe wowote ule kutoka kwenye picha na kuweka kwenye post zako zozote zile labda Whatsapp , Instagram , Facebook nk . Labda umeipenda ujumbe uliopo kwenye picha unahitaji kuchukua tumia Google lens tu.


5️⃣ Search for text or image from any physical documents or image 

Labda unataka kujua hii picha imetoka wapi unahitaji kupata picha ila Kuna maneno yapo ila wewe huyataki Yale maneno unahitaji picha tu basi kupitia Google lens utaweza kupata picha yoyote ile unayotaka kwenye mitandao mbalimbali.


Umeshawahi kutumia Google lens au ndo unasikia tuachie maoni yako? 


#josephleonard78

Post a Comment

0 Comments